SAFARI SIKU 1 NGORONGORO

MUHTASARI WA SAFARI

Alfajiri baada ya kifungua kinywa, tutaondoka na chakula cha mchana (Lunch box na vinywaji) na tutaelekea katika hifadhi ya Ngorongoro. Tutashuka kwenye Crater ya Ngorongoro kuchunguza tambarare yenye nyasi fupi za eneo la Crater kubwa zaidi ulimwenguni. Crater inafurahisha kwa haiba yake ya kudumu inayotokana na uzuri wake na wingi wa wanyama wa porini wanaokaa na kudumu ndani ya bonde la crater. Crater inajumuisha maili za mraba100 ikiwa na viumbe hai kama simba, chui, vifaru, tembo, nyati, na wengine wengi. Tutafurahia huko kwa mchana mzima na kupata chakula hukohuko mpaka mida ya karibia jioni ambapo tutaanza kurudi jijini Arusha au Moshi kulingana na ulipoanzia safari yako.

Baadhi ya utakayoyapata safarini.

 1. Utapata kuona wanyama wakubwa watano wa Afrika wajulikanao kama (The Big Five). Ikiwa una bahati unaweza hata kuona vifaru weusi.
 2. Utatembelea bwawa maarufu la kiboko na utakula chakula cha mchana huku ukipata kumbukumbu kwa kupiga picha ukiwa katika eneo hilo.
 3. Utatazama wanyama wa kawaida kwenye crater kama vile mbwa mwitu, tembo, nyati, punda milia, faru na swala wa aina mbalimbali.
 4. Utafurahia kuona vile ambavyo Crater kubwa duniani imewezesha maisha kwa viumbe hai wengi wanaopata mahitaji yao yote bila kutoka ndani ya eneo hilo ukizingatia Crater ilitokana na mlipuko wa Volcano.
 5. Utatembelea Ziwa Magadi na uangalie flamingo wa rangi ya pink na ndege wengine wengi.

BEI YA SAFARI

Wasiliana nasi moja kwa moja ili tukupatie mpango bora wa gharama na ulipaji wake.

Hapa chini tumeorodhesha nini hujumuishwa kwenye bei yetu ya safari na nini huwa havijumuishwi kwenye bei hiyo.

Vijumuishwavyo kwenye bei

 • Kodi zote za serikali.
 • Maji ya kunywa ya chupa.
 • Muongoza watalii azungumzaye Kiswahili.
 • Malazi na chakula wakati wote wa safari.
 • Ada zote za kuingia mbugani.
 • Usafi katika gari maalum la safari lenye mfumo wa 4×4

Visivyojumuishwa kwenye bei

 • Vinywaji vilevi.
 • Usafiri wa kutolewa na kurudihswa uwanja wa ndege.
 • Malazi kabla na baada ya safari.
 • ¬†Mahitaji mengine binafsi kama vile kamera, na bima ya safari.

WASILIANA NASI

Jaza fomu ifuatayo na mmoja wa wataalamu wetu wa safari atawasiliana nasi mara tuu tukipokea fomu hii.

Fomu ya kupata kupanga zaidi kuhusu safari

[Form id=”35″]