SAFARI SIKU 1 TARANGIRE

MUHTASARI WA SAFARI

Kwa kawaida huwa tunaondoka mjini Arusha saa moja kamili asubuhi, na kama ni kuanzia Moshi basi huwa ni saa kumi na mbili kasoro robo, kwa hiyo tunatarajia kuwa na utapata kifungua kinywa kabla ya kuondoka kwenye hoteli / nyumba ya kulala wageni utakayofikia au nyumbani kwako (kama ulilala nyumbani). Kuendesha gari kutoka Moshi kwenda Hifadhi ya kitaifa ya Tarangire ni takriban masaa 4, kwa hivyo tunapaswa kufika huko kati ya saa tatu na nusu hadi nne asubuhi.

Baada ya taratibu zote za kuingia hifadhini kukamilika tutaingia kuanza Game Drive muda wa masaa mawili na nusu, kisha mapumziko kwa chakula cha mchana muda wa saa 7mchana. Baada ya mapumziko ya chakula cha mchana, tutakuwa na lisaa limoja la Game Drive ndani ya hifadhi kabla ya kurejea Moshi au Arusha.

Tarajia kushuhudia yafuatayo:

 1. Miti ya Mibuyu – jitayarishe kusikia maelezo mafupi ya miti hii mikubwa zaidi ulimwenguni.
 2. Kiasi kikubwa cha ndovu/tembo na ujifunze juu ya wanyama hawa wa ajabu na wenye akili za ajabu.
 3. Mazingira ya Hifadhi ikiwa ni pamoja na mto wake wa ajabu ambao hutoa jina kwa hifadhi ya kitaifa, mto huo unaitwa mto Tarangire.
 4. Wanyama wawindao kama Simba na Duma wanapotafuta wanyama ambao huenda kutafuta maji kwenye mto wa Tarangire.
 5. 5.Aina nyingine nyingi za wanyama walao nyasi pamoja na ndege wa aina mbalimbali katika hifadhi ya Tarangire. (Yapo mengi ya kufurahiwa na kujifunza tuwapo Mbugani tarangire).

BEI YA SAFARI

Wasiliana nasi moja kwa moja ili tukupatie mpango bora wa gharama na ulipaji wake.

Hapa chini tumeorodhesha nini hujumuishwa kwenye bei yetu ya safari na nini huwa havijumuishwi kwenye bei hiyo.

Vijumuishwavyo kwenye bei

 • Kodi zote za serikali.
 • Maji ya kunywa ya chupa.
 • Muongoza watalii azungumzaye Kiswahili.
 • Malazi na chakula wakati wote wa safari.
 • Ada zote za kuingia mbugani.
 • Usafi katika gari maalum la safari lenye mfumo wa 4×4

Visivyojumuishwa kwenye bei

 • Vinywaji vilevi.
 • Usafiri wa kutolewa na kurudihswa uwanja wa ndege.
 • Malazi kabla na baada ya safari.
 • ¬†Mahitaji mengine binafsi kama vile kamera, na bima ya safari.

WASILIANA NASI

Jaza fomu ifuatayo na mmoja wa wataalamu wetu wa safari atawasiliana nasi mara tuu tukipokea fomu hii.

Fomu ya kupanga zaidi kuhusu safari

[Form id=”34″]