Safari hii ya siku tatu mbugani imeandaliwa rasmi kwa watanzania na watu wengine wanaozungumzia lugha ya Kiswahili. Muongozaji wako mbugani atazungumza kila kitu kwa Kiswahili ili mpate kuelewana vema nawe ufurahie na kujifunza mengi kutoka mbugani. Safari hii inajumuisha kulala katika maradhi karibu na hifadhi kwa siku moja ingawa utakua na siku mbili za kutalii mbugani. Utaanza safari kwa kuitembelea mbuga ya Tarangire kisha utaenda kuishuhudia mbuga bora zaidi ya zote barani Afrika, mbuga ya Serengeti. Utamalizia safari hii kwa katika hifadhi ya Ngorongoro.
Kwa kawaida huwa tunaondoka mjini Arusha saa moja kamili asubuhi, na kama ni kuanzia Moshi basi huwa ni saa kumi na mbili kasoro robo, kwa hiyo tunatarajia kuwa na utapata kifungua kinywa kabla ya kuondoka kwenye hoteli / nyumba ya kulala wageni utakayofikia au nyumbani kwako (kama ulilala nyumbani). Kuendesha gari kutoka Moshi kwenda Hifadhi ya kitaifa ya Tarangire ni takriban masaa 4, kwa hivyo tunapaswa kufika huko kati ya saa tatu na nusu hadi nne asubuhi.
Baada ya taratibu zote za kuingia hifadhini kukamilika tutaingia kuanza Game Drive muda wa masaa mawili na nusu, kisha mapumziko kwa chakula cha mchana muda wa saa 7mchana. Baada ya mapumziko ya chakula cha mchana, tutakuwa na lisaa limoja la Game Drive ndani ya hifadhi kabla ya kuelekea Karatu kwa chakula cha jioni na kisha kulala.
Muhtasari wa siku ya kwanza.
5.Aina nyingine nyingi za wanyama walao nyasi pamoja na ndege wa aina mbalimbali katika hifadhi ya Tarangire. (Yapo mengi ya kufurahiwa na kujifunza tuwapo Mbugani tarangire).
Kutoka Karatu kwenda hifadhi ya kitaifa ya Serengeti Baada ya kifungua kinywa baada ya malazi huko Karatu, Tutachukua Chakula cha mchana na maji (Lunch box) na kuanza safari ya masaa 3 kwenda hifadhi ya kitaifa ya Serengeti. Itakuwa safari inayopitia Ngorongoro.
Lengo letu katika siku hii ni kufika katikati mwa Serengeti,Tutaifurahia Serengeti kwa masaa yote yaliyobaki, kula chakula mchana na kulala humo humo mbugani. Tutapata chakula cha Jioni na malazi.
Muhtasari wa siku ya Pili.
Asubuhi baada ya kifungua kinywa tutaendelea kuitazama mbuga ya Serengeti kabla ya kuanza safari ya kuelekea Ngorongoro kuishuhudia crater kubwa zaidi ulimwenguni. Tutashuka kwenye Crater ya Ngorongoro kuchunguza tambarare yenye nyasi fupi za eneo la Crater kubwa zaidi ulimwenguni. Crater inafurahisha kwa haiba yake ya kudumu inayotokana na uzuri wake na wingi wa wanyama wa porini wanaokaa na kudumu ndani ya bonde la crater. Crater inajumuisha maili za mraba100 ikiwa na viumbe hai kama simba, chui, vifaru, tembo, nyati, na wengine wengi. Tutafurahia huko kwa mchana mzima na kupata chakula hukohuko mpaka mida ya karibia jioni ambapo tutaanza kurudi jijini Arusha au Moshi kulingana na ulipoanzia safari yako.
Muhtasari wa siku ya Tatu.
Wasiliana nasi moja kwa moja ili tukupatie mpango bora wa gharama na ulipaji wake.
Hapa chini tumeorodhesha nini hujumuishwa kwenye bei yetu ya safari na nini huwa havijumuishwi kwenye bei hiyo.
Vijumuishwavyo kwenye bei
Visivyojumuishwa kwenye bei
Jaza fomu ifuatayo na mmoja wa wataalamu wetu wa safari atawasiliana nasi mara tuu tukipokea fomu hii.
[Form id=”37″]